Ezekiel 19:4-8

4 aMataifa wakasikia habari zake,
naye akanaswa katika shimo lao.
Wakamwongoza kwa ndoana
mpaka nchi ya Misri.

5 b“ ‘Mama yake alipongoja na kuona tumaini lake halitimiziki,
nayo matarajio yake yametoweka,
akamchukua mwanawe mwingine
na kumfanya simba mwenye nguvu.
6 cAlizungukazunguka miongoni mwa simba,
kwa kuwa sasa alikuwa simba mwenye nguvu.
Akajifunza kurarua mawindo
naye akala watu.
7 dAkabomoa ngome zao
na kuiharibu miji yao.
Nchi na wote waliokuwa ndani yake
wakatiwa hofu kwa kunguruma kwake.
8 eKisha mataifa wakaja dhidi yake
kutoka sehemu zilizomzunguka.
Wakatanda nyavu zao kwa ajili yake,
naye akanaswa katika shimo lao.
Copyright information for SwhNEN